Baadhi ya wenye magari wakiwa wamekwama katika Kituo cha mafuta cha Big Bon Sinza Mori baada ya kukosa mafuta kwa muda mrefu katika vituo mbalimbali vya kuuzia mafuta jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa wafanyakazi wa kituo hicho usumbufu huo ulianza tangu saa tano asubuhi baada ya mafuta ya Petroli kumalizika na wahusika kwenda kufuata Mbagala bila mafanikio na kupata taafifa kuwa yanapatikana Kigamboni.
Wahusika waliamua kufuata mafuta hayo Kigamboni tangu mchana huo lakini mpaka sasa mida hii ya saa 2 na dakika 40 usiku bado wahusika hawajafika na kusababisha msongamano mkubwa mahala hapa, huku foleni ya magari ikifika hadi SInza kijiweni na Bamaga.
Katika Kituo hicho cha Big Bon, wanadai kuwa yanapatikana mafuta ya Diesel pekee lakini Petroli imeisha na bado uhakika wa kupatikana. Baadhi ya watu walisikika wakisema kuwa hivi sasa tayari hadi katika vituo vingine hayapatikani mafuta yote Diesel na Petrol na kufanya vituo hivyo kufungwa.
Baadhi ya magari yakiwa katika foleni ya kusubiri mafuta katika Kituo cha Big Bon, Sinza Mori, muda huu.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kituo hicho wakiwa wameketi hawana kazi ya kufanya kutokana na Pampu zao kuishiwa na mafuta.
Foleni ya magari......
Tax nyingine zilikuwa na abiria zikisubiri mafuta katika foleni.
No comments:
Post a Comment