BAADA ya mvua kubwa kuharibu baadhi ya Miundombinu na maeneo kadhaa ya Manispaa ya Iringa, sasa mvua hiyo imeamua kutoa sadaka ya kuangusha Senene na kuwafaidisha wakazi wa Manispaa hiyo, ikiwa ni pamoja na kumkaribisha Mkuu wa Mkoa mpya mwenye asili na Kitoweo hicho, Dkt, Ishengoma.
Mbali ya senene hao kugeuka mboga katika familia hizo bado baadhi ya vijana wasio na ajira wamejikuta wakipata kujiajiri wenyewe na kujipatia fedha kiasi baada ya kukusanya magunia kwa magunia ya senene na kuuza kati ya shilingi 15,000 hadi 20,000 kwa debe moja .
Viajana hao wameendelea kujipatia pesa ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya kwa kuchangamkia biashara hiyo ya msimu ambayo ni nadra sana kutokea kwa mkoa wa Iringa.Naye Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr.Christina Ishengoma ameonyesha kutokwa na mate wakati akifungua kikao cha bodi ya barabara mkoa katika ukumbi wa St Dominic baada ya kuona senene hao wakiwa wamezagaa ndani ya ukumbi huo na kushindwa kujizuia kueleza hisia zake dhidi ya Senene hao.
Vijana wakichangamkia biashara ya kupima Senene kwa wateja wao.
No comments:
Post a Comment