Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi kombe Mkurugenzi wa Mahusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steven Kilindo wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais za Mwaka 2011 za Mzalishaji Bora kwa wanachama wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI). Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Maofisa wa kampuni ya Bia Tanzania wakiwa katika picha ya Pamoja na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, baada ya kukabidhiwa vikombe kwa kushinda Tuzo za Rais za Mwaka 2011 za Mzalishaji Bora kwa wanachama wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI).
Maofisa wa kampuni ya Bia Tanzania wakiwa katika picha ya Pamoja baada ya kukabidhiwa kombe kwa kushinda Tuzo za Rais za Mwaka 2011 za Mzalishaji Bora kwa wanachama wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI).
Meneja Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi (shoto) akiwa na Meneja wa Mambo ya Nje wa kampuni hiyo, Emma Oriyo huku wakiwa na kombe lao.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
No comments:
Post a Comment