Habari za Punde

*FAINALI ZA MASHINDANO YA MITUMBWI 'BALIMI EXTRA LAGER' YAFANA

  Washiriki wa shindano la Mitumbwi 'Balimi Extra Lager' wakiwa majini wakichapa mwendo wakati wa shindano hilo lililofanyika eneo la Mwaloni jijini Mwanza jana.


  Na  Michael Machellah, Mwanza

NANSIO Ukerewe waibuka mabingwa  na kujinyakulia jumla ya Sh. Miliioni 4,800,000, katika Fainali za mashindano ya Mitumbwi ya Balimi Extra Lager yaliyomalizika jana eneo la Mwaloni Jijini Mwanza.

Fainali za mashindano haya yalikuwa ya Kanda ya ziwa ikishilikisha jinsia zote ya keke na kiume,ambapo Ukerewe waliibuka washindi kwa jinsia zote kwa wanaume kikundi cha Martin Mwarabu kutoka Nansio Ukerewe na kujipatia zawadi ya Shilingi Milioni 2,600,000, na kwa upande wa wanawake Kikundi cha Teddy Totto cha Nansio Ukerewe pia kiliibuka na ushindi na kuzawadiwa Shilindi milioni 2,200,000.

Matokeo hayo kiliyafanya mashndano kuwa na shamrashamra za kushangilia kwa aina yake kwa ngoma ndelemo na vigelegele toka kwa wakazi wa Ukerewe walitoka Ukerewe na Wakewe waishio Mwanza hivyo kukifanya Kitonjoji cha Mwaloni kujaa ndelemo na vifijo.

Mshindi wa pili kwa wanaume walikuwa ni kikundi cha Umoja kutoka Bukoba ambao walizawadiwa Shilingi 2,000,000, wa tatu ni kikundi cha Kisolya  kutoka Msoma ambao walizawadiwa Shilingi milioni 1,600,000 na wa nne ni kikundi cha Nyalusulya kutoka Musoma na washiliki wa tano hadi wa kumi walizawadiwa kifuta jasho cha Shilingi 400,000 kila kikundi, ambavyo ni Kanchakwizi kutoka Bukoba,Elisha Jacob cha Mwanza,Godfrey Ignatus chaNansio Ukerewe,Rwekaza kutoka Bukoba,Matinika Hangaika kutoka Mwanza na cha Shija Andrew kutoka Mwanza.

Mshindi wa pili kwa wanawake walikuwa ni kikundi cha Kinesi kutoka Musoma ambacho kilipata Shilingi 1,600,000,cha tatu ni kikundi Mfunda Mfunda Mbogo kutoka Mwanza na cha nne ni cha Happiness Mnare kutoka Mwanza na vikundi vingine cha tano hadi kumi walizawadiwa kifuta jasho Shilingi 200,000, kila kikundi ambavyo ni Rwagasire kutoka Musoma,Tindichebwa Mganga kutoka Mwanza,Busira kutoka Bukoba,Seleka kutoka Bukona,Paskazia Shukurani kutokaNansio Ukerewe na cha Elizabeth Charles kutoka Mwanza.

Mashindano hayo yalihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Evarist Ndikilo ambaye ndiye akikuwa mgeni rasmi akisindikizwa na Mkuu wa Wilaya, Said Amanzi na kiongozi mwenyeji kutoka Kampuni ya Bia Tanzani walikuwa ni Meneja wa Bia ya Balimi iliyodhamini mashindano, Edith Bebwa na Meneja mauzo na usambazaji wa Kanda, Malaki Staki.
  Sehemu ya wakazi wa Jijini Mwanza wakishuhudia mashindano ya Mitumbi ya Balimi Extra Lager Mwaloni Jijini Mwanza jana.
  Wakazi wa Jijini Mwanza wakishuhudia mashindano hayo.
 Washindi wa kwanza upande wa wanawake,Kikundi cha Teddy Totto kutoka Nansio Ukerewe wakiwasili Mwaloni wakati wa mashindano ya Mitumbwi Balimi Extra Lager yaliyomalizika.
  Washindi wa kwanza upande wa wanaume,Kikundi cha Martin Mwarabu kutoka Nansio Ukerewe wakiwasili Mwaloni wakati wa mashindano ya Mitumbwi Balimi Extra Lager yaliyomalizika jana.
Washindi wa kwanza upande wa wanawake wakikabidhiwa zawadi yao ya kitita cha Shilingi Milioni 2,200,000 ambao ni kikundi cha Teddy Titto kutoka Nansio Ukerewe.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.