Habari za Punde

*HILI NDILO LINALOFANYA MAGARI YA CHAI MAHARAGE KUENDELEA KUPIGA KAZI UNGUJA

Pamoja na Jitihada za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kujaribu kuyapiga marufuku magari aina ya Chai Maharage yanayotoa huduma ya kubeba abiria kutofika maeneo ya katikati ya mji, ili kuendana na mabadiliko ya Kiteknolojia ya ufasiri, Imeelezwa kuwa bado magari haya yataendelea kutoa huduma hiyo kinyemela kutokana na kuwa na uwezo wa kubeba mizigo mingi ya abiria wake tofauti na Daladala za sasa kama Hice Dungu na Double Coaster, ambazo hazina nafasi ya kubeba abiria na mizigo.

Wakizungumza na Mtandao huu wa Sufianimafoto kwa nyakati fofauti baadhi ya wakazi wa Mjini Unguja walisema kuwa wananchi waliowengi bado wanatumia magari hayo kutokana na wengi wao kutoka pembezoni mwa mji na mizigo yao ya biashara ambayo mingi inakuwa haitozwi pesa na kufikisha katikati ya mji kwa ajili ya kuuza katika Malkiti (Soko). 
Magari hayo yakipishana wakati yakiendelea kuchapa kazi katikati ya mji wa Zanzibar. Baadhi ya wananchi wameshauri kuwa magari hayo yaachwe yaendelee kutoa huduma ili yabaki kama ukumbusho wa Visiwani Zanzibar hadi hapo yatakapokuwa yakiisha yenyewe kutokana na kuchoka.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.