Salum Ally ama ukipenda kwa jina maarufu kwa jijini Dar es Salaam na katika baadhi ya mikoa ambayo hufanyia shughuli zake ni (Mzee Cuf), huyu yeye ni Mpiga picha maarufu wa picha za kuuza al-maarufu kama Picha za Manyaa.
Picha za Banyaa ni zile picha zinazopigwa katika shughuli yeyote ikiwa ni Mkutano ama sherehe bila mpigwaji kuwa na mkataba na mpigaji na kisha huletewa picha ikiwa tayari na kuuziwa.
Mzee Cuf, kwa upande wake pamoja na
kuwa ni maarufu zaidi katika fani ama ujuzi wa kupiga picha lakini yeye amekuwa bado hadi hii leo haamini Kamera zinazoendana na mabadiliko ya Teknolojia yaani kamera za 'Digital', kiasi kwamba hadi leo hii bado anaamini kwa kufanya kazi na kamera yake aliyokwishaizoea ya Nikkon ya kutumia Filim.
Akizungumza na Mtandao wa Sufianimafoto, Mzee Cuf, aliyewahi kushiriki katika mchakato wa kumuondoa Nduli Idd Amin Dada katika Mipaka ya Tanzania, mwaka 1978, anasema kuwa pamoja na kuwa mkakamavu kutokana na kuwahi kuwa 'Mjeda' Afande wa Jeshi la JWTZ na kushiriki Vita ya Kagera lakini bado anaamini hatua kubwa ya maisha yake imetokana na Kamera ambayo hadi hii leo anaitumia kwa kupiga picha za Banyaa na kumwezesha kujipatia kipato chake cha kila siku cha kuitunza familia yake pamoja na matumizi ya kawaida yanayohitajika katika familia.
"Kamwe sitaweza kuacha kamera hii na kurukia katika hizo zenu za Bongo Flava, akimaanisha kamera za Digital, kwani naiamini sana kamera hii ya mknda kuliko hata hizo zinazowarahisishia mambo,
Unajua kamera hizo ni sawa na Gari la Auto ambalo hata mlemavu ama mtoto anaweza kuendesha kwa maelekezo kidogo tu, lakini gari ya Manu hata awe mtu mzima ni lazima aende shule ndiyo aweze kuliondoa gari" alisema Mzee Cuf.
Kwa mujibu wa Mzee Cuf mwenyewe, alishiriki katika Vita ya Kagera akiwa katika Kikosi cha Kakunyu No, 824 kilichokuwa chini ya Captain Alenguya.
Mzee Cuf, akipozi kwa picha na kamera yake akiwa katika moja ya hafla za Kitaifa miaka ya nyuma, (kulia) ni Mpiga picha wa Waziri Mkuu wa sasa, Hirary Bujiku.
Mzee Cuf akiwa katika moja ya pori wakati akiwa katika Vita ya Kagera, kwa mujibu wa Mzee Cuf ilikuwa ni Agost 24, 1978.
Mzee Cuf (kulia) akiwa na mwenzake, wakiwa katika harakati za vita ya Kagera, 1978.
No comments:
Post a Comment