Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI HAFLA YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA WA KIISLAM WA 1433

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba wakati wa halfa ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislam iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiqaama Tanzania Tawi la Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika leo, katika Ukumbi wa Karimjee jijini.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Msaafu kutoka kwa, Sheikh Ahmed Mohamed Lbadry, baada ya kumaliza hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislam iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiqaama Tawi la dare s Salaam  na kufanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini.
  Waumini wakiomba dua baada ya kumalizika hafla hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakati akiondoka kwenye Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam, leo .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alilopata nalo ajali Bw. Arif Yusuph, eneo la Mji wa Fiche Kilometa 100 kabla ya kufika Adis Ababa , wakati akitoka Kuhij Makha baada ya kugongana uso kwa uso na gari aina ya Hice iliyokuwa imebebea Jeneza ikisafirisha msiba, katika ajali hiyo watu wote walisalimika na kurejea nyumbani. Makamu wa Rais alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislam iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiqaama na kufanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waumini na viongozi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Istiqaama, baada ya kumalizilika kwa hafla hiyo leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.