Habari za Punde

*OKWI AACHA MAUMIVU KILIMANJARO STARS WASHINDA 3-1

Timu ya Uganda leo imeiadhibu timu ya Kilimanjaro Stars kwa mabao 3-1 katika hatua ya Nusu Fainali katika mchezo uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo Kilimanjaro Stars ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza kupitia mshambuliaji wake machachari, Mrisho Ngasa katika kipindi cha kwanza bao lililodumu hadi timu hizo zilipokwenda mapumziko.

Kipindi cha pili Uganda ilikuja juu na kuandika bao la kusawazisha kupitia Beki wake Mwesigwa aliyepanda na kufunga mpira wa kichwa kufuatia mpira wa kona na kufanya timu hizo kumaliza dakika 90 zikiwa sare ya 1-1 na kwenda katika dakika 30 za nyongeza kabla ya mchezaji,Emmanuel Okwi,kuongeza maumivu kwa kufunga bao safi kwa kichwa na baadaye kusababisha penati iliyoipatia Uganda bao la tatu na la ushindi katika mchezo huo.

Kwa matokeo hayo sasa Uganda itavaana na Rwanda katika Fainali za michuano hiyo siku ya Jumamosi, huku Kilimanjaro Stars ikimenyana na Sudan iliyochapwa na Rwanda mabao 2-1 katika kuwania nafasi ya tatu ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.