Habari za Punde

*POLISI DRC WADAIWA KUUA RAIA 24 KINSHASA, BAADA YA UCHAGUZI ULIOTAWALIWA NA DOSARI

KUNDI la kutetea Haki za Binadam la Marekani, limesema katika ripoti yake kuwa Wafuasi wa Tshisekedi DRC,wamesema kuwa polisi wa nchini humo wanadaiwa kuua raia takriban 24 baada ya uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo tangu kufanyika kwa uchaguzi uliotawaliwa na dosari kadhaa.

Rais K abila waliapishwa kushika madaraka kwa awamu ya pili wiki hii, lakini mpinzani wake mkuu, Etienne Tshisekedi alikataa kuyatambua matokeo ya uchaguzi huo, huku akiendelea kusisitiza kuwa na yeye atajiapisha siku za hivi karibuni baada ya kukamilika kwa maandalizi ya sherehe yake hiyo.
Shirika la Human Rights Watch (HRW) lilisema vifo vingi vimetokea katika mji mkuu Kinshasa, ambako Tshisekedi ana watu wengi wanaomuunga mkono.
 
Lilisema lina ushahidi vikosi vya usalama vimejaribu kufunika vifo hivyo.

Uchaguzi huo ulitayarishwa kwa mara ya kwanza nchini humo tangu nchi hiyo imalize vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2003, vilivyosababisha watu milioni nne kuuawa.

Matokeo yalitangazwa Disemba 9 lakini mpinzani wake Bw Tshisekedi akakataa kuyatambua mara moja na wanaomuunga mkono wakiongoza vurugu mjini Kinshasa.

Waangalizi wa kimataifa kutoka nchi za magharibi walisema mchakato wa uchaguzi ulijaa dosari nyingi kukubalika.

HRW lilisema vifo hivyo na ukamataji wa watu ‘kiholela’ wa watu wengi ilionekana kuwa ni hatua ya serikali kujaribu kuzuia upinzani dhidi ya matokeo hayo.

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia na kuzungumza na wafanyakazi wa HRW na wanaharakati wa Kongo kundi hilo linasema lina ushahidi wa watu 20 ambao waliuawa mjini Kinshasa, wawili Kivu ya Kaskazini na wawili katika jimbo la Kasai Occidental.

Miongoni mwa waathirika wanaotajwa ni watu wa upinzani waliojaribu kupinga au hata watazamaji akiwemo kijana mdogo wa miaka 13 aliyepigwa risasi akiwa amesimama nje ya nyumba yao na mwanamke aliyeuawa wakati anatafuta watoto wake.

"Hatua hiyo ilichafua mchakato wa uchaguzi na kuacha picha kuwa serikali ingelifanya lolote linalowezekana kukaa madarakani," alisema Anneke Van Woudenberg, mtafiti mwandamizi wa HRW Afrika.

HRW linasema vikosi vya usalama vilionekana kufunika kiwango cha mauaji kwa kuondoa miili na kuwaambia wafanyakazi wa afya wasitoe habari kuhusu vifo hivyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.