Habari za Punde

RAIS KIKWETE, LEO AMUAPISHA BALOZI SEFUE KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI, BADALA YA LUHANJO

 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha rasmi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, kuwa Katibu Mkuu Kiongozi badala ya Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, aliyemaliza muda wake. Hafla hiyo ya kumuapisha Balozi Sefue, imefanyika leo Ikulu Dar es Salaam. Wa pili (kushoto) kwa Rais ni Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phllemon Luhanjo, akisimamia zoezi hilo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiingia katika ukumbi wakati wa hafla fupi ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, aliyeapishwa  na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salaam leo.
  KATIBU Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, ni Manataaluma ya Dipromasia ambaye tokea Agosti 31, 2010, amekuwa mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani.

Kabla ya kuteuliwa kwenda kuwa mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, Balozi Sefue, alikuwa ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani katika mji wa Washington DC tokea Juni 15, 2007. Na kabla ya hapo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada, nafasi aliyoishikilia tangu Oktoba 2005 hadi Juni 2007.
Sefue, pia amewahi kuwa Ofisa Mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden katika Mji wa Stockholm kati ya mwaka 1987 na 1992.
Kati ya mwaka 1993 na 2005, Sefue, alikuwa ni mwandishi wa hotuba na msaidizi binafsi wa Marais wawili, Rais Ali Hassan Mwinyi  (1993-1995) na Rais Benjamin Mkapa (1995-2005).

Miongozni mwa mambo mengine, Balozi Sefue alimsaidia Rais Mkapa wakati alipikuwa Kamishna wa Afrika (kwenye Kamisheni ya Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo, akiwa ni Tony Blair), ambapo alitoa ripoti iitwayo, ‘Our Common Interest,  Ripoti  of the Commission for Africa’, mwezi Machi mwaka 2005, na pia alishiriki kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za G8, ambao ulijadili ripoti hiyo ambao ulifanyika Gleneagles, Scotland mwezi Julai mkwa 2005.

Aidha Balozi Sefue, alifanya kazi na Rais Mkapa wakati Mheshimiwa Mkapa alipokuwa Mwenyekiti mwenza wa Kamisheni ya Shirika la Kazi Duniani ya ILO World Commission, iliyojadili masuala ya Kijamii ya Utandawazi kati ya mwaka 2002 na 2004, ambapo alishiriki katika maandalizi ya ripoti ya Kamisheni hiyo iitwayo, A Fair Globalisation Creating Opportunities For All, iliyotolewa mwzi Februari mwaka 2004.

Balozi Sefue, alipata Elimu yake ya Juu katika Chuo Kikuu cha Mzumbe (ambacho kwa sasa ni Chuo Kikuu cha Mzumbe) katika masuala ya Utawala mwaka 1997.

Pia alipata Shahada ya Uzamili katika masuala ya Sera na Utawala kutoka Institute of Social Studies (ISS) mjini The Hague, Uholanzi mwaka 1981.
Alipata Diploma ya Juu katika Chuo cha Diploma cha Dar es Salaam mnamo mwaka 1986, na pia Balozi Sefue alimuoa Mama Anita M. Sefue na anawatoto wawili.   
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, wakipiga picha ya pamoja baada ya hafla ya kuapishwa rasmi kwa katibu huyo leo Ikulu Dar es Salaam.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue na Balozi Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, wakizungumza jambo baada ya hafla ya kuapishwa rasmi kwa katibu huyo leo Ikulu Dar es Salaam
 Rais Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, wakipiga picha ya pamoja na Makatibu wakuu, baada ya hafla hiyo ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi iliyofanyika leo Ikulu Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue (kushoto) akifurahia jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, wakati wa hafla hiyo ya kuapishwa katibu Mkuu kiongozi Ikulu Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, akihojiwa na waandishi wa habari, mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue Ikulu Dr es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.