Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini ( TANROADS ) Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) pamoja na Meneja Mkazi wa Kampuni ya Mkandarasi M/S STRABAG INTERNATIONAL GmbH ya Ujerumani, Heribert Schippers, (kulia) wakitiliana saini mkataba wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mfumo wa Usafiri Haraka wa Mabasi jijini Dar es Salaam awamu ya kwanza, Kandarasi wa Kwanza (Barabara) wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Ujenzi. Mradi huo wa Ujenzi unafadhiliwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia ambapo mradi mzima utagaharimu shilingi Bilioni 240.9 ,ujenzi wa awamu ya kwanza unahusisha ujenzi wa barabara unaofikia kilometa 20.9 katika barabara ya Morogoro (kutoka Kimara hadi Kivukoni Feri), barabara ya Kawawa (kutoka Magomeni hadi Morocco ) na barabara ya Msimbazi (kutoka Fire hadi makutano ya Nyerere -KAMATA). Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli , Viongozi wa TAMISEMI, Wizara ya Fedha na wadau mbalimbali wa sekta ya Ujenzi. Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli, akionyesha ramani yya baadhi ya michoro ya barabara za juu (Flying- Over) zitakazojengwa jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano na waandishi wa habari na Wadau wa sekta ua Ujenzi leo, wakati ya hafla ya uwekaji wa sahihi ya Mradi wa ujenzi wa miundombini ya mfumo wa Usafiri haraka wa mabasi jijini Dre salaam-awamu ya kwanza, Kandarasi ya kwanza (barabara), utakapo kamilika ujenzi wa barabara hizo itasaidia kupunguza msongamano wa magari jijini.
No comments:
Post a Comment