WAKATI jumla ya sh. Milioni 55 zimechangishwa katika maonyesho ya mitindo kwa ajili ya kuadhimisha siku ya ugonjwa hatari wa UKIMWI duniani (Red Ribbon Fashion Gala), mwanamuziki nyota nchini, Diamond aling’ara vilivyo kwa kuonyesha kipaji kingine cha maonyesho ya mavazi.
Fedha hizo zilipatikana kwa njia ya mnada wa vitu mbali mbali na nyingine zikitolewa kwa njia ya udhamini wa shughuli hiyo iliyotumika pia kuadhimisha siku ya ugonjwa hatari wa Ukimwi Duniani.
Mwanamboka alisema kuwa kituo hicho kitajengwa jijini na kitatoa mafunzo ya njia mbali mbali za kupambana na maisha, Ujasiliamali, Ushonaji nguo, mafunzo ya kompyuta na jinsi ya ubinifu wa mitindo au mavazi.
Alisema kuwa jumla ya watoto yatima 100 watakuwa wanapata mafunzo katika kituo hicho kila mwaka.
Baadhi ya wadhamini waliochangia kufanikisha kwa fedha hizo ni kampuni ya simu ya mkononi, Vodacom Tanzania na wadau wa maonyesho ya mavazi ambao walichangia kimya kimya katika maonyesho hayo yaliyofanyika kwenye hotel ya Double Tree.
Katika maonyesho hayo, mkali wa miondoko ya Bongo Fleva nchini, Diamond naye alifanya vitu vyake jukwaani kwa kuvaa nguo aina ya Kidoti iliyobuniwa na mbunifu chipukizi, Jokate Mwegelo.
Wengine walioonyesha mavazi jukwani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Production, Ritha Poulsen ambaye baadaye nguo yake iliunuliwa na mcheza filamu maarufu nchini, Steven Kanumba.
Wadhamini wengine wa shughuli iyo walikuwa Redds, Clouds Entertainment, Kiondo Communications, I_View Media team na Hall Neel Production. Wengine waliosaidia maonyesho hayo ya mavazi ni Amaya Beauty Saloon and SPA, Bank M Tanzaniia, Stanbic Bank, Mimis collections, Kidoti By Jokate Mwegelo, Bongo Real Mamaz na Bluecherriemoe.
Wadau wengine ni Flaviana Matata Foundation, Amina Design, Jenifa Pemba, FM Express events and services ltd, Ernst &Young, ,LR Creations, Millen Magese Foundation Tiffex, Cool Blue Iku Lazaro, Miraj Kikwete, Halima Kamus, Mabibo Beer Wines nd Spirits Ltd, and World Link Travel and Tours ltd.
No comments:
Post a Comment