Habari za Punde

UBALOZI WA TANZANIA UINGEREZA WATANGAZA HABARI NJEMA KWA WATANZANIA

Wakati wa kuadhimisha Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara Ubalozi wetu hapa nchini Uingereza wakishirikiana na Chuo kikuu cha mji Coventry wanapenda kuwatangazia wadau wote wa elimu kuwepo kwa Scholarship sita maalum za masomo kwa watanzania ambazo zimetolewa kutoka katika Chuo kikuu cha Coventry katika nyanja zifuatazo:

1. MSc Oil & Gas Management

Coventry Campus

Kuanzia Septemba 2012

2. MBA Oil & Gas Management

London Campus

Kuanzia April, July, Septemba 2012

3. MSc Finance & Investment

IAA Dar Campus

Kuanzia Septemba 2012

4. MBA Logistics

IAA Dar Campus

Kuanzia Septemba

5. MSc Finance & Investment

IAA Arusha Campus

Kuanzia Septemba 2012

6. MBA Logistics

IAA Arusha Campus

Kuanzia Septemba 2012

Jinsi ya kujiandikisha, tembelea tovuti ifuatayo hapo chini:
Mbali na hapo Ubalozi wetu ukiwakilishwa na Balozi Mh Peter kallaghe, Chabaka Kilumanga na Allen Kuzilwa walipata fursa pekee ya kukutana na kumpongeza afisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ndg. Semu Mwakyanjala ambaye pia ni mwanafunzi wa shahada ya Pili( Masters Degree in Communication, culture & Media) katika chuo kikuu cha Coventry alieshinda tuzo ya kuandika insha kuelezea jinsi gani nchi ya Ujerumani itakavyokua mwaka 2051.

Aidha Mh. Balozi Kallaghe alimpongeza sana Afisa Semu kwa juhudi zake kwa kufanikiwa kushinda tuzo hii na kuiletea heshima Tanzania Ughaibuni na kuwahamisisha watanzania wote kusoma na kufanya kazi kwa bidii zaidi. Wakati akiongea na waandishi wa Habari afisa Semu alianza kwa kutoa shukrani kwa familia yake, wafanyakazi wenzake kutoka TCRA na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa kumwezesha kufikia hatua aliyopiga leo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na ubalozi wetu hapa London 00 44 20 7569 1470

Tafadhalini watanzania wote chukueni hii nafasi mapema iwezekanavyo kwa wale wote mnaopenda kujiendeleza kimasomo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.