Habari za Punde

*VODACOM MISS TANZANIA AKABIDHIWA GARI LAKE AINA YA JEEP LEO

  Vodacom Miss Tanzania Salha Isarel akipokea funguo ya gari aina ya Jeep Patriot, kutoka kwa Meneja Matukio na Udhamini wa kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa, wakati wa hafla fupi ya  makabidhinao ya zawadi ya mrembo huyo aliyetwaa taji la Vodacom Miss Tanzania 2011,  katika shindano la Taifa lililofanyika Septemba. Kulia ni Mkurugenzi wa Lino Agency waratibu wa shindano hilo la Vodacom Miss Tanzania, Hashim Lundenga na (kushoto) ni Meneja Masoko wa CFAO wadhamini wenza wa shindano hilo, Alfred Minja. Gari hiyo ina thamani ya shilingi  Milioni 72.
 Vodacom Miss Tanzania Salha Isarel akionyesha funguo ya gari aina ya Jeep Patriot lenye thamani ya shilingi milioni 72 kwa furaha baada ya kukabidhiwa na Meneja Udhamni na Matukio wa kampuni ya Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa (wa pili kulia).
Meneja Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi rasmi zawadi ya Vodacom Miss Tanzania 2011, Salha Israel. Kulia ni Meneja Masoko wa CFAO Alfred Minja ambao ni wadhamini wenza wa shindano la Vodacom Miss Tanzania.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.