Habari za Punde

*RAIS JAKAYA KIKWETE AWASILI KAMPALA KUHUDHURIA MKUTANO WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU KUPINGA UNYANYASAJI NA UKATILI WA KIJINSIA

 Rais Jakaya Kikwete, akiwasili kweny Uwanja wa Ndege wa Entebe Jijini Kampala Uganda kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu kuhusu kupinga Unyanyasaji na Ukatili wa Kijinsia, ulioanza leo jijini humo. Picha na Ikulu
 Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na maofisa wa Tanzania waliohudhuria mkutano huo baada ya kuwasili kwenye Ukumbi wa mkutano huo.
 Rais Jakaya Kikwete (kulia) akizungumza na Rais wa Zambia ambaye ni Mwenyekiti wa ICGLR aliyemaliza muda wake, Michael Chilufya Sata (kushoto) na Rais wa kenya Mwai Kibaki, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu wenye lengo la kupinga Unyanyasaji na Ukatili wa Kijinsia, ulioanza leo jijini Kampala Uganda.
 Rais Sata na Mwenyekiti waICGLR, akimkabidhi Rais wa Uganda, Museven, ikiwa ni ishala ya  kumkabidhi madaraka ya 'kuchair' kiti hicho cha Mkutano huo wa Nchi za Maziwa Makuu ulioanza leo Jijini Kampala Uganda kuhusu kupinga Unyanyasaji na Ukatili wa Kijinsia.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba (wa tatu kushoto) akiwa  na baadhi ya wadau wa mkutano huo wakati ukiendelea jijini Kampala Uganda leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.