Habari za Punde

*WAUNGWANA MDAU ANAOMBA MSAADA KUMTIBU MWANAE



Bi. Sharifa Juma (31) mkazi wa Tanga mjini (pichani), anawaomba watanzania wenye mapenzi mema kumwezesha ili mwanae mwenye ulemavu wa uti wa mgongo aweze kupatiwa matibabu katika hospitali yoyote hapa nchini au nje ya nchi.
Mwanane Feisal Alawi (miezi 9) alipata matatizo ya uti wa mgongo mara baada ya kuzaliwa na mpaka sasa hawezi kukaa wala kutambaa.
Amewahi kumpatia matibabu katika Hospitali ya watoto wenye matatizo ya viungo ya CCBRT ya jijini Dar es Salaam lakini kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha alishindwa kuendelea na matibabu hayo. Kwa sasa mtoto Alawi anahitaji kupatiwa mazoezi ya kukaa kwenye kiti maalum na kupatiwa matibabu ya mifupa ili kukomaza uti wa mgongo.
Yeyote anakayeguswa na taarifa hii atume msaada wake kwenye A/C No. 010-00033092 ya Benki ya Posta Tawi la Metropolitan Dar es Salaam au awasiliane naye kwa Namba 0714 735 322.
Na pia unaweza kusaidia hata kwa njia ya Tigo Pesa chochote ulichojaaliwa kumsaidia, kupitia namba hiyo iliyoandikwa hapo juu. Mungu atakubariki.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.