Habari za Punde

*BREAKING NEEEEEWZ! MBUNGE MSTAAF, GALINOMA AFARIKI DUNIA

 Marehemu Stephen Galinoma
Habari za uhakika zilizotua katika mtandao huu kutoka Kalenga katika wilaya ya Iringa vijijini zinadai kuwa mbunge wa zamani wa jimbo la Kalenga Mhe.Stephen Galinoma pichani amefariki dunia asubuhi hii wakati akikimbizwa katika hospitali teule ya wilaya ya Iringa hospitali ya Ipamba .
Habari ambazo mtandao huu umezipata na kuthibitishiwa na mtoto wa Galinoma Magreth zinadai kuwa Galinoma amefariki majira ya asubuhi ya leo wakati akikimbizwa hospital hiyo ya Ipamba .
Alisema kuwa marehemu kabla ya kifo chake alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo na taarifa zaidi utaendelea kuzipata katika mtandao huu .
Marehemu Galinoma alikuwa mbunge wa jimbo la Kalenga kupitia CCM kuanzia mwaka 2005 hadi 2010 alipostaafu na nafasi yake kuchukuliwa na mbunge wa sasa Dr Wiliam Mgimwa .

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.