Habari za Punde

*H-BABA AKAMILISHA KIBAO KIPYA CHA SINA RAHA, AMPA SHAVU BANZA STONE

H-Baba katika pozi
MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini, Hamis Ramadhan ‘H-Baba’ amekamilisha kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la Sina Raha, akimshirikisha gwiji wa muziki wa dansi nchini, Ramadhan Masanja, ‘Banza Stone’ Mwalimu  wa Walimu.
Akizungumza na Mtandao wa Sufianimafoto, H-Baba, alisema kuwa kibao hicho ni miongoni mwa nyimbo zake 10 zitakazokamilisha albam yake mpya itakayokwenda kwa jina la ‘Shika hapa acha Hapa’ inayotarajia kuingia sokoni mwezi wa tatu mwaka huu.
Aidha alisema kuwa wimbo ambao amemshirikisha Banza Stone, amerokodia katika Studio ya Allan Mapigo, ambapo tayari amekamilisha maandalizi ya kurekodi video ya wimbo huo mwishoni mwa wiki hii.
H-Baba alisema kuwa katika wimbo huo mashabiki wake watarajie kupata vitu tofauti ikiwa ni pamoja na staili mpya na midundo iliyo ‘shiba’ na sauti murua ya Banza Stone, aliyeonyesha uwezo wake katika wimbo huo.
Alizitaja studio alizorekodia nyimbo zake zitakazokamilisha albam hiyo kuwa ni pamoja na KGC Studio, Maneke Studio na Allan Mapigo, zote za jijini Dar es Salaam.
Pia alizitaja baadhi ya nyimbo zitakazokuwamo katika albam hiyo kuwa ni pamoja na, Nipe Kidogo, Shika Kichwa, Kinacho Niumiza, Zaidi yako Wewe na Nimpende Nani.
  

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.