Habari za Punde

*KIJITONYAMA VETERANS LEADERS KUKIPIGA LEO KUWASINDIKIZA MSONDO NGOMA

Na Mwandishi Wetu, Dar
TIMU ya soka ya Kijitonyama Veterans leo inapambana na timu ya maveteran wa Leaders Club, Leaders Club FC katika mchezo maalum wa kirafiki wa kusindikiza sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mchezo huo umepangwa kuanza saa 10.00 jioni kwenye uwanja wa Leaders Club na utasindikizwa na burudani safi ya bendi ya Msondo Ngoma “Baba ya muziki” chini ya udhamini wa Konyaji kwa mujibu wa mratibu wa Kijitonyama Veterans, Majuto Omary.
Majuto alisema kuwa mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na timu zote kuundwa na wachezaji bora. Alisema kuwa kitu kingine kinachofanya mchezo huo kuwa wa aina yake ni rekodi za timu mbili katika mechi zake za hivi karibuni.
Kijitonyama Veterans ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa bonanza la maveterani lililoandaliwa kwa ajili ya kutimiza miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania kwa kutofungwa hata mechi moja tokea kuanzishwa kwake katikati ya mwaka uliopita.
Leaders Club ilifanikiwa kushika nafasi ya pili ya mashindano maalum yaliyoandaliwa kwa ajili ya uzinduzi wa albamu ya Dunia Daraja Novemba 5 mwaka jana. “Ni mchezo wa aina yake na Kijitonyama Veterans ambayo ipo katika mikakati ya kufanya ziara mikoa ya Kanda ya Kaskazini itakuwa na wachezaji wake nyota kama Kiki De Kiki “Tom Mawejje”, Hamis Kayuga “Chumvi”, Saidi “Mihogo” Seif na Isahaq Said ‘Niyonzima’.
Leaders Club itakuwa chini ya Sammy Tabu, Adam Mkwawa, Ninja, Steve NyerereMalaga, na kiongozi wao Japhet Tibenda.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.