Pages

Karibuni Katika ukurasa wa Sufiani Mafoto, jipatie Habari Motomoto na Matukio Mbali Mbali yanayojiri kila siku.Pia Tunakaribisha Matangazo Ya Aina mbalimbali kwa gharama Nafuu Kabisa.Kwa mawasiliano +255 655 306 109.Nyote Mnakaribishwa.

Tuesday, January 24, 2012

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AANZA ZIARA YA MKOA WA TANGA LEO, AKAGUA UKUTA WA KUZUIA MAJI YA BAHARI , AZINDUA OFISI YA IDARA YA MAJI, PANGANI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ukuta unaozuia maji ya Bahari eneo la Pangani Kivukoni, unaozidi kubomoka kutokana na kujengwa miaka 100 iliyopita na kutishia amani kwa wakazi wa maeneo hayo.  Makamu wa Rais ameanza ziara yake ya Mkoa wa Tanga jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Pangani wakati akitoka kukagua ukuta wa kuzuia maji ya  Bahari unaobomoka Pangani Kivukoni.
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Jengo la Ofisi ya Idara ya Maji, lililopo Wilaya ya Pangani, wakati alipoanza ziara yake ya Mkoa wa Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa (kushoto) ni Mkurugenzi wa Maji wa wilaya hiyo, Mohamed Hamis.

0 idadi ya maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA BLOG