Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA MASHAMBA YA MPUNGA YA KOROGWE, AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA UKUMBI NA OFISI YA HALMASHAURI YA KOROGWE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wakulima wa Mpunga kuhusu kilimo hicho cha umwagiliaji wakati alipotembelea na kukagua mashamba ya Skim Mamlaka ya mji wa Mombo jana.
 Wakulima wa mashamba hayo wakiimba na kushangilia ujio wa Makamu wa Rais shambani hapo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Viongozi wa Wilaya ya Korogwe, wakikagua jengo la Ukumbi na Ofisi ya Halmashauri ya Korogwe baada ya kuweka jiwe la Msingi katika jengo hilo alipokuwa kwenye ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya wilaya hiyo jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Kombe, Kiongozi wa timu ya Mombo Shooting, Mohamed Dassa, kwa ajili ya timu hiyo iliyopanda daraja kutoka Ligi ya Ngazi ya Wilaya na kuingia Ligi Ngazi ya Mkoa. Kombe hilo pamoja na vifaa vya michezo vimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Steven Ngonyani ‘Maji Marefu’.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.