Waziri Mkuu Mizengo Pinda, tayari amekabidhi Sh. milioni 10 kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ikiwa ni ahadi yake aliyotoa kwa Taifa Stars ikiwa ni motisha kwa wachezaji wa timu hiyo kabla ya mechi yao na Chad iliyochezwa Novemba Mosi mwaka jana jijini N’Djamena.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Meneja wa Taifa Stars, Leopold Tasso linaandaa orodha ya wachezaji wanaostahili kunufaika na ahadi hiyo, na baadaye kuiwasilisha BMT kwa ajili ya mgawo kwa wahusika.
TFF tunamshukuru Waziri Mkuu Pinda kwa ahadi hiyo, kwani Taifa Stars ilifanikiwa kushinda mechi hiyo ya ugenini mabao 2-1, ushindi ambao bila shaka ulichagizwa na ahadi hiyo.
No comments:
Post a Comment