Habari za Punde

*ZIARA YA MAKAMU WA RAIS DKT BILAL MKOANI LINDI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Daraja la Mingumbi lililopo Wilaya ya Kilwa, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Mkoa wa Lindi jana. Kushoto ni mkewe, Mama Zakhia Bilal (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovic Mwananzila.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Ilulu, baada ya kuzindua rasmi Jengo la Bwalo la shule hiyo, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Mkoa wa Lindi jana.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakishangilia wakati Makamu akiwahutubia jana.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.