Watu wasiopungua 37 wameuawa Sudan Kusini katika vurugu za upiganaji risasi kwenye mkutano wa amani unaolenga kumaliza ghasia katika eneo hilo.
Wakitoa taarifa hiyo maofisa kutoka majimbo matatu waliokutana katika mazungumzo yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa katika mji wa Mayendit, kwenye jimbo la Unity, katika jitihada za kupunguza uhasama wa kikabila.
Kwa mujibu wa taarifa hizo kutoka Umoja wa Mataifa zinazohusiana na ghasia, Sudan Kusini, mzozo ulizuka na magari manne kuwasili yakiwa yamejaa polisi ambao mara moja walianza kufyatua risasi.
Miongoni mwa waliokufa ni raia. Wanaharakati wa haki za binaadam wameshutumu ukosefu wa nidhamu miongoni mwa majeshi ya usalama.
Mazungumzo hayo yaliitishwa kufuatia mfululizo wa mapigano, yakiwemo mapigano ambayo watu 74 waliuawa mapema wiki hii.
Mamia ya watu wamekimbia makazi yao kutokana na ghasia hizo.
No comments:
Post a Comment