Mshambuliaji wa Timu ya Ivory Coast na mfungaji wa bao pekee katika mchezo huo, Gervinho (katikati) akipambana kuwatoka wachezaji wa Maali, Seydou Keita (kushoto) na Samba Diakité (kulia) wakati wa mchezo wa Kombe la Mataifa ya Afrika uliomalizika hivi punde katika Uwanja wa de l'Amitie Libreville.
Nahodha wa timu ya Ivory Coast, Didier Drogba (kushoto) akichuana kuwania mpira na Nahodha wa Mali, Cedric Kante, wakati wa mchezo wa Kombe la Mataifa ya Afrika uliomalizika hivi punde katika uwanja wa de l'Amitie Libreville.
Mchezaji nyota maarufu wa zamani wa Brazil, Pele, akiingia uwanjani kwa mbwembwe huku akipunga mkono kuwasalimia mashabiki wa soka 'akitroti' kabla ya kuanza kwa mchezo wa nusu fainali baina ya Ivory Coast na Mali, mchezo uliomalizika hivi punde kwa Ivory Coast kuibuka na ushindi.
**********************************
IVORY Coast sasa itakutana na Zambia kwenye fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya timu hizo mbili kushinda mechi zao za nusu fainali hii leo.
Ivory Coast imefuzu baada ya kuichapa Mali katika mchezo wa nusu fainali yao mjini Libreville, nchini Gabon.
Katika mchezo wa mwanzo uliochezwa katika mji wa Bata nchini Gabon Zambia nayo iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ghana kutoka mashindano.
Bao la Zambia lilifungwa katika dakika ya 78 na mshambuliaji Emmanuel Mayuka.
Katika kipindi cha kwanza mshambuliaji wa Ghana Asamoah Gyan alikosa kufunga penalti, baada ya mlinda mlango wa Zambia kuutema nje mpira.
Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika itachezwa siku ya Jumapili mjini Libreville, nchini Gabon.

No comments:
Post a Comment