Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia kalenda aliyozawadiwa na Jaji Mkuu Mh. Mohamed Chande Othman baada ya kuhutubia katika Siku ya Sheria Tanzania jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na viongozi wa Baraza la Taifa la NGOs Ikulu jijini Dar es salaam leo kuzungumzia mchakato wa Katiba.
SALAMU ZA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWENYE SIKU YA
SHERIA
Mheshimiwa Jaji Mkuu, Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;Mheshimiwa Jaji Mkuu wa Zanzibar; Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria; Mheshimiwa Jaji Kiongozi na Majaji wa Mahakama Kuu;Mheshimiwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika; Mahakimu na Watumishi Wengine wa Mahakama; Wageni Waalikwa; Mabibi na Mabwana: Nakushukuru sana Mheshimiwa Jaji Mkuu kwa kunialika kuja kujumuika nanyi katika siku hii adhimu ya kuadhimisha Siku ya Sheria kwa mwaka 2012.
Nakushuru pia kwa kunipa nafasi ya kutoa salamu kwa hadhara hii ya mabingwa wa sheria na watoaji haki.
Lazima nikiri kuwa baada ya kusikiliza nasaha maridhawa zilizotolewa katika hotuba yako nzuri na nyinginezo za walionitangulia mimi sintokuwa na mengi
ya kusema.
Hakika tumepata darasa la kutosha. Hivyo, nitasema machache.
Niruhusuni nianze kwa kutakiana heri ya Mwaka Mpya.
Naungana na viongozi wa dini waliotuombea dua hapa leo hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuumaliza mwaka uliopita salama na tunamuomba atujaalie neema na baraka tele mwaka huu wa 2012.
Tumuombe atujaalie ndoto zetu zitimie na tunayopanga yafanikiwe.
Mheshimiwa Jaji Mkuu; Nakupongeza sana wewe binafsi kwa kazi yako nzuri uifanyayo ya kusimamia na kuuongoza mhimili wa Mahakama. Wahenga walisema ‘nyota njema huonekana asubuhi’. Katika kipindi kifupi ulichokuwa
Jaji Mkuu umeonyesha kuwa wewe ni kiongozi mahiri na mtetezi.
shupavu wa maslahi ya mhimili wa Mahakama na haki za raia.
Aidha,
umekuwa daraja imara kati ya mihimili yetu mitatu ya dola yaani
Serikali, Bunge na Mahakama. Kupitia kwako, mafanikio mengi
yamepatikana na heshima na taswira ya Mahakama katika jamii inazidi
kuboreka. Nakushukuru sana.
Nawapongeza, pia, Majaji wa Rufaa, Majaji wa Mahakama Kuu,
Mahakimu pamoja na watumishi wengine wote wa Mahakama. Kwa
kweli wamefanya kazi kubwa na nzuri pamoja na kuwepo changamoto
mbalimbali. Mimi na wenzangu Serikalini pamoja na wananchi walio
wengi tunatambua na kuthamini mchango wenu muhimu katika utoaji
wa haki. Jitihada zenu ndizo zimewezesha Mahakama kupata
mafanikio ambayo tunayazungumzia leo. Mimi naamini kuwa
mwelekeo wetu wa siku za usoni unaleta matumaini makubwa.
Ujumbe wa Mwaka
Mheshimiwa Jaji Mkuu;
Nawapongeza sana kwa mada nzuri ya maadhimisho ya Siku
ya Sheria mwaka huu inayosema “Adhabu Mbadala Katika Kesi
za Jinai na Faida zake katika jamii”. Kwa hakika huu ni ujumbe
ambao umekuja wakati muafaka kabisa.
Jambo hili ni muhimu sana. Ni ukweli ulio wazi kwamba
mfumo wetu wa sasa wa adhabu unasisitiza adhabu ya kifungo jela
badala ya adhabu mbadala ambazo zipo katika sheria. Kama adhabu
mbadala zingekuwa zinatolewa, idadi ya wafungwa gerezani
ingepungua na hata tatizo la msongamano katika magereza
lisingekuwepo au lingepungua sana.
Hatuna budi kutumia adhabu mbadala kama sheria ya The
Community Act inavyoruhusu kwa makosa yanayostahili. Sheria hiyo
inajenga dhana kwamba jukumu la kuwarekebisha wahalifu haliko
mikononi mwa Serikali pekee na kwamba jamii wanakotoka wahalifu
nayo ina wajibu wa kushiriki katika kuwarekebisha wahalifu. Sheria ya
kufanya kazi ya kijamii ililenga kuwaepusha na adhabu ya kifungo wale
3
Check Against Delivery
wafungwa ambao wameonyesha tangu awali kwamba waliteleza,
wametubu na kuomba msamaha.
Utekelezaji wa sheria hizi una changamoto zake ambazo
Mheshimiwa Jaji Mkuu umezieleza kwa ufasaha. Moja ya changamoto
hizo ni ile ya jamii kukubali ukweli kwamba wahalifu wanarekebishika.
Adhabu zinazotolewa zina lengo la kumrudi na kumrekebisha mhalifu.
Inapodhihirika kuwa mwenendo wa mhalifu una muelekeo mzuri na
hasa unapopima uzito wa kosa alilofanya ni dhahiri kwamba ni kwa
manufaa ya mfungwa kurekebishwa na jamii badala ya kumtenga kwa
kumfunga gerezani. Hii ni namna nyingine ya kumpa mhalifu fursa ya
kujirekebisha katika jamii yake.
Hata hivyo, kuna changamoto ya jamii kutambua na kukubali
kuwa inao wajibu mkubwa katika kusaidia kuwarekebisha wahalifu.
Naelewa ugumu uliopo kwa jamii kulielewa jambo hili kwani wengi
wanaamini kwamba adhabu pekee ya mhalifu ni kumfunga gerezani.
Hivyo, ipo kazi kubwa ya kutoa elimu ili watu nao waelewe kuwa
wanao wajibu wa kusaidia kuwarekebisha wafungwa wawe na tabia
njema.
Mheshimiwa Jaji Mkuu;
Changamoto nyingine ni jinsi jamii itakavyojipanga kufanya kazi
ya kuwarekebisha wahalifu katika jamii zao. Ingefaa wadau muhimu,
kama vijiji, Halmashauri na Mamlaka nyingine wabuni kazi na kutenga
maeneo ya kufanya kazi zenye manufaa kwa umma. Kazi hizo zisiwe
za kukwaza, bali ziwe za kuwarekebisha wahalifu. Ni muhimu kwa ajili
hiyo basi, Wakuu wa Mikoa, Wilaya na viongozi wengine wa Serikali za
Mitaa wakahusishwa kwa ukamilifu katika utekelezaji wa adhabu
mbadala. Tukifanya hivyo mpango huu utakuwa umepewa msukumo
wa pekee na kupata mafanikio.
Kuhusu suala la msongamano wa wafungwa, baada ya kutembelea
magereza ya Keko, Ukonga na Segerea na kuyaona niliyoyaona,
nimeshawishika tuchukue hatua. Nimetoa maagizo kwa wahusika
kuandaa maoni yao. Baadhi wamekamilisha na wengine wanamalizia.
No comments:
Post a Comment