Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA MAGHARALA MAWLI YA KUHIFADHIA BIDHAA KTK BANDARI YA KASANGA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika moja ya jengo kati ya mawili ya Maghala ya kuhifadhia Bidhaa yaliyopo katika Bandari ya Kasanga, kijiji cha Lusambo Wilaya ya Sumbawanga, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi na Rukwa jana.

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATEMBELEA KAMBI YA KASANGA YA KIKOSI CHA ULINZI WA MIPAKA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozwa na Luteni Godfrey Semiono (Mkuu wa Kambi) kukagua kikosi cha Ulinzi wa Mipaka cha Kasanga kilichopo katika kijiji cha Lusambo, pembezoni mwa Wilaya ya Sumbawanga, wakati alipofika eneo hilo kwa ajili ya kuzindua maghala ya kuhifadhia bidhaa katika Bandari ya Kasanga jana, wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Katavi na Rukwa
  *MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AWATEMBELEA WAFANYA BIASHARA WA SAMAKI KTK SOKO LA KASANGA, BAADA YA KUWEKA JIWE LA MSINGI.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea kukagua maeneo ya kufanyia biashara ya baadhi ya wafanyabiashara wa samaki katika Soko la Samaki la Kasanga, baada ya kuweka jiwe la msingi katika soko hilo akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi na Rukwa, jana
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuwaaga wananchi wa Kijiji cha Lusambo waliojitokeza katika mapokezi yake alipofika kuweka jiwe la msingi katika Soko la Kasanga, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi na Rukwa jana.
MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA JENGO LA OFISI YA MAMLAKA YA MAPATO SUMBAWANGA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe, Mama Asha Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Ofisi ya Mamlaka ya Mapato TRA baada ya kuzindua jengo hilo lililopo Sumbawanga.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.