Sufianimafoto, hapa nikiwa kandokando ya Ziwa Tanganyika katika Bandari ya Kasanga Kijiji cha Lusambo Wilaya ya Sumbawanga, katika ziwa hili raia wa nchi za Tanzania na Malawi hufaidika na Samaki wa Migebuka wanaopatikana katikaziwa hili, ambapo raia wengie wa Malawi huvuka kutoka upande wa pili na kufuata kitoweo anga hizi huku na raia wa Tanzania wakivuka kwenda kuuza samaki wao katika fukwe za Malawi.
Lakini sasa tayari Serikali imetatua tatizo hili kwa kujenga soko la kisasa la Samaki la Kisanga, ambapo wafanyabiashara wote wa samaki wameaswa kuuzia samaki wao katika soko hilo na kuwavutia raia wa kigeni kufika katika soko hilo kununua samaki hao kwa bei iliyopangwa tofauti na awali ambapo wafanyabiashara walikuwa wakinyonywa kwa kupunjwa bei za samaki hao kwa kuamua bei wanazohitaji wao.
No comments:
Post a Comment