Bi Clinton akizungumza na wanahabari
.
MAREKANI imesema kuwa mataifa ya kirafiki yanayoitakia Syria utawala wa Kidemokrasia yanapaswa kuungana katika kumshutumu kiongozi wa taifa hilo Rais Assad.
Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa mashauri ya Kigeni wa Marekani, Bi Hillary Clinton, alisema ni jambo la kusikitisha kuwa Urusi na Uchina zilipiga kura za turufu kupinga azimio la kuikosoa Syria katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Aidha alitoa wito kwa jamii ya kimataifa iunge mkono makundi ya upinzani nchini Syria.
Ni wazi kwamba Marekani pamoja na wanadiplomasia wa mataifa mengine ya Magharibi
wameghadhabishwa mno na hatua ya Urusi na Uchina kupinga azimio la kuikosoa Syria.
Bi Clinton aliyasema hayo wakati akiwa nchini Bulgaria ambako amesema Marekani pamoja na mataifa mengine zitashinikiza rais Assad aondoke madarakani.
Pia alizungumzia kuhusu kuwekwa kwa vikwazo zaidi kwa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwataja watu ambao wanafadhili wakuu ambao wanaipa silaha serikali ya Syria.
No comments:
Post a Comment