Habari za Punde

*MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA WAADHIMISHA SIKU YA WADAU KWA KUTOA MSAADA WA MASHUKA 700 KWA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA MKOANI MBEYA

 Naibi Mkurugenzi Mkuu wa  NHIF,  Hamis  Mdee, akitoa msaada wa Mashuka kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha  Ruanda kinachotoa huduma kwa kinamama Wajawazito, Eliot Sanga, wakati ujumbe huo ulipofika katika kituo hicho kukabidhi misaada msaada huo leo Jijini Mbeya.
 Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF,  Mariam More, akikabidhi sehemu ya mashuka kwa ajili ya baadhi ya Wodi za Hospiali hiyo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika leo jijini Mbeya.  Jumla ya Mashuka 700 yalikabidhiwa katika hafla hiyo leo.ANAYEPOKEA KATIBU WA AFYA WA HOSPITALI HIYO BI DORICE NZIGIRWA
   Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHIF, Mariam More (kushto) akitandika moja ya shuka katika kitanda kilichopo Wodi ya Wazazi kwenye Hospitali ya Igawilo baada ya kukabidhi msaada wa mashuka.ANAYEMSAIDIA NI NESI MWANDAMIZI BI DORICE MWAKABENGA.
Huyu si Mume Bwege bali ni mume anayeelewa majukumu ya Familia vilivyo, huu ni mfano bora kwa wanaume ulioonyeshwa na kidume huyu aliyejulikana kwa jina la Gibson Mwalibwa, akiwa na mtoto wake mgongoni wakati akitoka kupata huduma ya afya katika kituo hicho leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.