Bondia mahiri wa mchezo wa Kick Boxer, aliyepata kujizolea sifa lukuki katika mchezo huo kwa kuwasambaratiza wanadada wenzake kadhaa katika mchezo huo, Pendo Njau, Baada ya kuwa nje ya Ulingo kwa kipindi cha misiku chache zilizopita amepata mtoto baada ya kuwa nje ya ulingo kwa kipindi cha miezi kadhaa kutokana na kuwa mjamzito, hivi sasa anatarajia kurudi ulingoni kwa kishindo baada ya kujifungua salama.
Akizungumza na Mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, Pendo alisema kuwa hatua aliyoifikia yeye kwa hivi sasa ya kuwa na mtoto ni hatua muhimu ambayo kila binadamu aliyekamilika hupaswa kuifikia.
Aidha Pendo alishindwa kuweka bayana kuhusiana na baba wa mtoto wake na kudai kuwa muda utakapofika basi atafunguka zaidi na kuweka mambo hadharani. Akielezea mikakati yake ya sasa atakaporeje upya, Pendo alisema kuwa tayari amekwishaanza mazoezi madogomadogo ya kujiweka fiti, na baada ya kuwa fiti atakuwa tayari kupambana na Bindia yeyote atakayejitokeza kuomba kucheza naye.
No comments:
Post a Comment