Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA MAADHIMISHO YA WIKI YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (VETA) KITAIFA MKOANI TANGA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua mashine ya king’ola kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo,  Kitaifa mkoani Tanga.
 Makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia viatu na kusikiliza maelezo kuhsu utengenezaji wa bidhaa hiyo kutoka kwa Deogratias John (kushoto)  wa Chuo cha Waleavu cha Usariva Moshi, wakati akitembelea katika mabanda ya maonyesho alipozindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo Kitaifa mkoani Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Kapteni Mstaafu, Chiku Galawa. Wa pili (kushoto) ni Mkurugenzi wa VETA, Mhandisi. Zebadiah Moshi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi na mwasisi wa Chuo cha Gemmologiacal and jewelry Vocation cha Arusha, Peter Salla, kuhusu matumizi yam awe ya madini, wakati akitembelea katika mabanda ya maonyesho alipozindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo, Kitaifa mkoani Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Kapteni Mstaafu, Chiku Galawa. Wa pili (kushoto) ni Mkurugenzi wa VETA, Mhandisi. Zebadiah Moshi.
 Watoto walioiva katika Sanaa ya kupiga vyombo katika kundi maalum la Chuo cha VETA, wakitoa burudani kwa kupiga wimbo maalum wa kumkaribisha Makamu wa Rais Viwanjani hapo leo, lakini pamoja na udogo wa watoto hawa bado waliweza kuwashangaza watu waliofika mahala hapo kwa kumudu vyema kupiga vyombo hivyo.
 Hapa wakiimba kwa staili ya kupuliza matarumbeta...
 Madogo wakiendelea kuchapa mzigo na kuwaacha watu hoi.....
Hata Madereva waliokuwa wakiendelea na mafunzo ya udereva walifika viwanjani hapo kuwaletea wenzao msosi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.