Habari za Punde

*MWANAMUZIKI WA FM ACADEMIA ALFABE KABEZA 'AFULIA MBAYA' AOMBA MSAADA KWA WADAU

Alfabe Kabeza wa kwanza (kulia) akiwa na wanamuziki wenzake wakati alipokuwa na bendi ya Fm Academia.
*******************************
MWANAMUZIKI mahiri aliyekuwa wa bendi ya Fm Academia, Alfabe Kabeza, aliyepata kutamba na kibao chake mahiri cha Acha Tamaa, ametangaza rasmi kuomba msaada ili awekeze kujikimu kimaisha kutokana na hali yake ya kifedha kuzidi kuwa mbaya zaidi kila kukicha.

Kabeza aliyasema hayo wakati alipokutana na watangazaji wa kipindi cha 'Yaliyomo Yamo' kinachorushwa na Redio One, ambapo watangazaji hao walipanga kufanya naye kipindi cha 'Live' ili watu waweze kumsaidia kwa njia yeyote.

Aidha watangazaji hao Hanifa na mwenzake walidai kuwa mwanamuziki huyo aliwapa kila ukweli kuhusu yeye na kusema kuwa kwa hivi sasa anaishi Gesti mitaa ya Kinondoni, ambako hulipa Sh. 7,000 kwa siku, ambayo pia huipata kwa taabu sana tena kwa kupewa na washkaji ambao hukutana nao kama zali, wengine buku, buku tano maisha yanasonga.

Mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, ulimsaka Kabeza na kuchonga naye mitaa ya Kinondoni na kufunguka zaidi kuwa hivi sasa maisha yake yamekuwa ni ya kubangaiza zaidi na kushindwa kupanga nyumba kutokana na kuwa na kipato kidogo zaidi kisichoendana na uhalisia
wa maisha yake na kupanda kwa gharama za pango za nyumba jambo ambalo hana uwezo wa kulipa kiasi cha kuanzia 120,000 hadi 300, 000 kwa mwezi kwa ajili ya pango la nyumba.

Kabeza pia alikanusha vikali kuhusu uvumi uliotapakaa kuwa anazushiwa kuwa amekuwa 'CHIZI', ambapo alisema kuwa siku za nyuma aliugua malaria na si uchizi kama ambavyo amekuwa akizushiwa na watu.

''Ila hivi sasa sina hata mawasiliano yaani SIMU kwani nimefulia mbaya kiasi ilibidi niuze simu yangu ili niweze kupata mahitaji mengine, hivyo nawaomba mashabiki wangu wanisaidie kwa kile watakachojaaliwa ili niweze kuendesha maisha yangu.

Na pia nawaomba sana Mapedezyee wa mjini wanisaidie kunidhamini ili niweze kuingia studio kurekodi kazi zangu ambazo nyingi nimeshazikamilisha, kasoro ni mapene tu, na pia natafuta Meneja ili aweze kunisimamia katika kazi zangu niweze kurejea katika hali yangu ya zamani''. alisema Kabeza.

Baadhi ya maneno yaliyokuwamo katika kibao cha Acha Tamaa ni:- Acha Tamaaa mwanangu eeh! alinikanya Mama aliyenizaa, Jichunge yeye alisema nami...

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.