MABONDIA Seleman Gavile, wanatarajia kuzichapa Aprili 9 mwaka huu kuwania MKANDA wa ubingwa wa ngumi za kulipwa wa TPBO (Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa) pambano linalotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam.
Mpaka sasa Mkanda huo bado upo wazi, ambapo mabondia hao watapanda ulingoni katika uzito wa kg 75 middle weight.
Akizungumza kuhusu maandalizi ya Dar es Salaam na mtandao wa juu ya maandalizi yake Galile alisema amejiandaa vyema kwa ajili ya kunyakua mkanda huo ambao upo wazi kwa sasa.
"Naendelea kufanya mazoezi yangu kwa ajili ya kuwania mkanda huu ambao ninaamini utaweza kunitambulisha ubora wangu katika tasnia hii ya masumbwi," alisema Galile.
Alisema kuhusu mpinzani wake Mashali hana hofu naye kwa kuwa mchezo huo huamua nani mkali atakayetwaa ubingwa wakati wakiwa ulingoni na si nje ya hapo na kwa sasa nimepata staili mpya za mabondia wa dunia.
Katika Mchezo huo kutakua na DVD za maf
unzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa Kimataifa wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.
Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye,Lenox Lewis,Evalnder Holfilder na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi
No comments:
Post a Comment