Mabondia Francis Cheka (kushoto) na Mada Maugo, wakifurahia wakati wakishikilia mkanda wao watakaoupigania katika pambano lao la ubingwa. Hafla hiyo ya kutambulishwa mkanda imefanyika leo jijini Dar es Salaam.*******************
Na Mwandishi Wetu, jijini Dar
MABONDIA Francis Cheka na Mada Maugo, leo wametambulishwa rasmi na waandaaji wa pambano la ubingwa wa IBF na kuonyeshwa mkanda huo ambao utashindaniwa Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
Pambano hilo litakalokuwa la uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC) ambapo mwamuzi na majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.
Akizungumza na mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa pambano hilo, Kaike Siraju alisema kuwa kuwekwa wazi kwa mkanda huo kunaashiria kukamilika kwa maandalizi ya pambano hilo, ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo.
"Tunauanika mkanda ili kuwathibitishia wadau wa ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa tupo makini na pambano hili na sio la kibabaishaji na kama tulivyosema awali kuwa majaji watoka nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe kulingana na hadhi ya mkanda," alisema Kaike.
Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa siku hiyo hiyo ya pambano baada ya kutangazwa mshindi na kuvishwa mkanda wake wa ubingwa.

Awali mabondia hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanyika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hayo na kuandaliwa pambano la marudiano lililofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo pia Cheka, aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.
Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia alitangaza kugoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D', alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
"Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi", alisema Super D.
No comments:
Post a Comment