Habari za Punde

*SPIKA WA BUNGE ASEMA VIONGOZI WA BUNGE WATAKIWA KUTAMBUA MAJUKUMU YAO

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda,  akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Semina Elimishi kwa wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge na Kamati ya Uongozi katika hoteli ya White Sands jijini Dares Salaam leo.
*****
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
VIONGOZI wa Bunge wametakiwakuafuatamajukumuyaoyakazi, maadilinakufahamumipakayakeyakiutendajiilikuepushamigogoroinayowezakutokea.
 Kaulihiyoilitolewaleo(jana)  naSpikawa Bunge la JamhuriyaMuunganowa Tanzania,Anne 
Makinda wakati akifungua semina elimishi ya siku mbili yawajumbe waTume yaUtumishi wa Bunge na Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati ya Uongozi wa Bunge  inayoendelea katika hoteli ya White Sands jijini Dares Salaam.

Alisema kuwa Bunge ni mojawapo yamihimili ya dola na ni  chombo muhimu katika uongozi na hatma ya nchi yetu,
hivyo umuhimu wa chombo hicho ni sharti uendane na maadili ya viongozi wake.

“Ufanisi waTaasisi ya Bunge
unategemea utendaji kazi wa vyombo hivi viwili kwasababu vyombo hivi viwili ndiyo washauri wakuu wa spika katika kuliongoza Bunge ,” alisema Spika Makinda.

Aliongeza kuwa Kamati ya Uongozi ndicho chombo chenye mamlaka ya kumshauri Spika kuhusu hoja na masuala mb
alimbali yatakayowasilishwa Bungeni, ambapo kwa upande waTume yaUtumishi wa Bunge ndiyo kiungo kikuu cha Utawala na Usimamizi wa huduma mbalimbali zitolewazo kwa wabunge na watumishi wa Bunge .

Aidha Spika Makinda aliongeza kuwa vyombo hivyo viwili vinategemeana,
hivyo ni muhimu kukutana ili kubadilishana mawazo na uzoefu wa namna ya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Aliwataka viongozi hao kuwa wazi na huru katika majadiliano ya mada zitakazowasilishwa.
Spika Makinda alizitaja mada zitakazowasilishwa kuwa ni tano ambazo ni maadili, uongozi na utawala bora, majukumu ya Tume yaUtumishi wa Bunge na Kamati ya Uongozi na Mahusiano yake, taratibu za kiutendaji na mifumo ya mawasiliano Serikalini, nafasi ya mbunge katika uongozi,
itifaki na usalama, ikiwamo mahusiano ya mihimili mitatu (Bunge,
Utawala na mahakama katika uongozi wa nchi.

Naye Mbunge waJimbo la Kilindi, Beatrice
Shellukindo, alisema semina hiyo itawasaidia kuelewa majukumu yapi yanatakiwa kutekelezwa na vyombo hivyo viwili.

 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.