Baada ya kupindua nchi na kumng'oa madarakani Rais Amadou Toumani Tour, Wanajeshi hao walioasi nchini Mali wametangaza kuwa tayari wamezivunja Taasisi zote za Serikali na kusitisha mikataba yote.
Wanajeshi waasi wametangaza katika televisheni ya taifa ya Mali kuwa wamechukua udhibiti wa nchi, saa kadha baada ya kuvamia kasri ya rais.
Wanajeshi walioasi wanasema kuwa wamepiga marufuku ya kutotoka nje katika nchi nzima na kwamba katiba ya nchi hiyo haitatumika kwa sasa.
Siku ya Jumatano wanajeshi hao walifyatuliana risasi na wanajeshi watiifu wa Serikali.
Wanasema serikali haijawapa silaha za kutosha kukabiliana na waasi wa jamii ya Tuareg.
Tayari walikuwa wamechukua udhibiti wa kituo cha taifa cha redio na televisheni na kusitisha matangazo.
Baada ya saa kadha ya kuonyesha picha za nyimbo za wanamuziki wa Mali, kundi la wanajeshi likaonekana kwenye televisheni mapema jana, wakitambulishwa kama "Kamati itakayorudisha Demokrasia na kutuliza hali katika nchi".
Msemaji wa waasi hao, aliyetajwa kwa jina la Luteni Amadou Konare, alisema sasa wamemaliza "utawala usio thabiti" wa Rais Amadou Toumani Toure.
No comments:
Post a Comment