Habari zilizoufikia mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, zinaeleza kuwa Wafanyabiashara wa Masoko ya mjini Morogoro, leo wameanza mgomo wao wa kutofungua vibanda na kufanya biashara kwa kile wanacholalamikia kupandishiwa ushuru mara dufu na Halmashauri ya Morogoro.
Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu, mmoja kati ya wafanyabiashara hao aliyejitambulisha kwa jina la Hamza Ramadhan, alisema kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya kuona malalamiko yao yakipuuzwa na Uongozi wa Halmashauri kupiga danadana kila kukicha kukutana na kufanya mazungumzo.
Aidha Hamza, alisema kuwa Ushuru huo umepanda kutoka kiasi cha Sh.3000 hadi 10,000 kwa Vibanda na Sh. 10,000 hadi 50,000 kwa Viosk, jambo ambalo linapingwa na wafanyabiashara hao, ambao wamedai kuwa gharama hizo zilipandishwa ghafla.
No comments:
Post a Comment