Habari za Punde

*UN YAENDESHA WARSHA KWA MAOFISA WA MAWASILIANO WA SERIKALI YA ZANZIBAR

 Waziri wa nchi ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dr. Mwinyihaji Makame,  akizungumza wakati akifungua warsha ya maofisa mawasiliano wa Wizara husika mjini Zanzibar leo. Katikati ni kaimu mwakilishi wa UN Zanzibar Bi. Ruth Leano na kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alberic Kacou.
 Baadhi ya Wanamawasiliano wa serikali ya Zanzibar wakifuatilia kwa makini warsha hiyo.
 Baadhi ya Wanamawasiliano wa serikali ya Zanzibar wakifuatilia kwa makini warsha hiyo.
  Ofisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Hoyce Temu akiteta na Mheshimiwa Waziri Mwinyihaji Makame.
Kaimu Mwakilishi wa UN Zanzibar Bi. Ruth Leano na naye aliwakilisha program za UN zilizopo Zanzibar.
************************************

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
SHIIKA la Umoja wa Mataifa Tanzania kupitia kundi la maafisa mawasiliano linalojulikana kama United Nations Communication Group (UNCG), limeendesha warsha ya siku moja mjini Zanzibar kwa maafisa mawasiliano wa serikali ya Zanzibar wanaofanya kazi katika wizara zote za Zanzibar.

Warsha hiyo ilihudhuriwa na maafisa 40 wa wizara husika na ilihusu jinsi gani ya kuwawezesha wanamawasiliano wa serikali ya Zanzibar na UN kuimarisha mawasiliano yanayohusu maendeleo ya Jamii, hususan ya Zanzibar.
 Mheshimiwa Dr. Mwinyihaji Makame, waziri wa nchi ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar alifungua warsha hiyo. Julai 2011, UN pamoja na serikali ya Tanzania ilisaini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Msaada wa Maendeleo wa miaka minne (UNDAP).
Mpango huu umelenga kufanya kazi kwa pamoja na serikali ya Tanzania. Utoaji wa warsha kwa maafisa Mawasiliano wa serikali ni moja ya mikakati ya kuimarisha utoaji taarifa wa maendeleo ya programu zinazofanywa kwa pamoja ambapo kundi la Mawasiliano la UN litakutana na wanamawasiliano wa bara mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.