Habari za Punde

*WANAHABARI WA MKOANI IRINGA KUANDAMANA JUMANNE KUFIKISHA UJUMBE KWA UONGOZI WA MKOA

Na Francis Godwin, Iringa
WANAHABARI wa mkoani Iringa leo wamekutana na kupanga kufanya maandamano ya amani siku ya jumanne kupinga hatua ya uongozi wa mkoa wa Iringa kutumia ziara za viongozi wa kitaifa kunyanyasa wanahabari .

Hatua hiyo imekuja baada ya baada ya uongozi wa mkoa kuwalaza nje wanahabari hao wakati wa ziara ya Rais Kikwete wilaya ya Njombe na ziara ya Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghirib Bilal, aliyefanya ziara yake katika wilaya ya Makete, Njombe, Mufindi na Iringa hivi karibuni.

Akitoa taarifa hiyo mbele ya wanahabari katika viwanja vya bustani ya Manispaa ya Iringa leo mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Daud Mwangosi, alisema kuwa wanahabari wamekuwa ni watu wa kutetea makundi mbali mbali katika jamii ila wao wamekuwa nyuma kujitetea hata pale wanaponyanyasika.

.Hivyo alisema wakati umefika kwa wanahabari kuanza kufunguka na kudai haki zao pale zinapoonekana kupokwa na watu wachache kwa masilahi yao.

Aidha alisema kuwa mkoa wa Iringa na vyombo vyake umekuwa ukiongoza kwa kuvibagua vyombo vya habari wakati wa ziara za viongozi wa kitaifa na wakati mwingine kuwataka wanahabari hao kuchangia gharama za ziara hizo iwapo wanataka kushiriki ziara husika.

Mwangosi alisema kuwa imekuwa ni kawaida kwa ofisi ya mkuu wa mkoa kupitia Ofisa habari wake Denis Gondwe, kutoa mialiko kwa wanahabari hasa pale mkoa unapohitaji kufikisha taarifa mbali mbali kwa wananchi ila inapotokea ziara za viongozi wa kitaifa ama mkuu wa mkoa kufanya ziara amekuwa akibagua vyombo vya habari na kutumia chombo cha serikali pekee.

''Lakini mwisho wa siku maandamano hayo yanaweza kuleta picha tofauti kwa baadhi ya watu na kuwashangaza walio wengi kutokana na utaratibu ambao kila chombo kimejiwekea kuhusiana na upatikanaji wa HABARI,

Ikiwa ni pamoja na Chombo husika kumuandalia kila kinachohitajika wandishi wake ili kuweza kufanikisha kupata habari, lakini pia katika utaratibu wa mazoea ya waandishi walio wengi na hasa wa mikoani, Uongozi wa Mkoa pia unamapungufu iwapo kweli walitoa kauli kama ambazo zimeelezwa kani Mikoa mingine huwaandalia wanahabari usafiri kuanzia mwanzo wa ziara hadi mwisho na mambo mengine,

Ni wakati sasa wa kukaa chini na walalamikaji hao na kuzungumza nao na kurekebisha pale palipokosewa ili kuweza kusonga mbele na kulijenga Taifa kwa kila mmoja katika nafasi yake na kwa ushirikiano na umoja, isiwe mwandishi akahitajika pale tu anapohitajika kumtumika kwa maslahi binafsi na kuwanufaisha wengine huku yeye akibaki kuwa kama DARAJA la kuwavusha watu siku zote''. Haya ni mawazo ya Mtandao huu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.