MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha
leo imetangaza rasmi kumvua Ubunge aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini, Godbless Lema kwa
tiketi ya CHADEMA.
Hukumu ya kesi hiyo iliyokuwa ikimkabili Lema kufuatia kutoa maneno machafu ya kumdhalilisha mpinzani wake kupitia CCM, Dkt. Batilda Burian, ambaye kwa sasa ni Balozi ya Tanzania nchini Kenya, imetolewa na Jaji
Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika hukumu ya kesi yhiyo a kupinga matokeo ya Ubunge
Jimbo la Arusha hilo yaliyo wasilishwa na wanachama watatu wa CCM
waliotaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ushindi wa Mbunge
huyo.
Wana CCM hao waliofungua kesi hiyo ni pamoja na Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Molle (44).
Wana CCM hao waliofungua kesi hiyo ni pamoja na Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Molle (44).
Kuvuliwa Ubunge kwa Lema, kutatonesha na kuzima furaha za Chama chake ambacho bado kipo katika shamra shamra za ushindi wa
Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki mkoani humo.
Pia habari za ndani ya Chama
cha Chadema zinasema kuwa tayari Chama hicho kilisha soma alama za nyakati
mapema katika kesi hiyo miezi kadhaa nyuma na kujipanga endapo mbunge huyo
atavuliwa wadhifa wake nani atasimamishwa kutetea kiti hicho.
Habari hizo zinadai kuwa
Chadema kimepanga kumsimamisha Katibu Mkuu wa Chama hicho na Mgombea Urais wa
2010, Dk. Wilbroad Silaa kutetea kiti hicho.
Aidha Wanachama hao wanadai kuwa taratibu za maadili ya
uchaguzi zilikiukwa kuwa mshindi alitumia lugha za kashfa, matusi na kejeli
katika mikutano ya kampeni aliyofanya jimboni Arusha.
Katika kesi hiyo wadai walileta mashahidi 14
kwenda kutoa ushahidi wao katika mahakama hiyo na wadaiwa walifanikiwa kuwaleta
mashahidi 5 kujitetea.

No comments:
Post a Comment