Msemaji wa pambano laa Ngumi kati ya Mada Maugo na Francis Cheka , Yasini Abdallah, akionyesha mkanda na Gari atakalopewa mshindi wa pambano jilo, linalotarajia kufanyika Aprili 28, mwaka huu kwenye Ukumbi wa PTA Temeke, jijini Dar es Salaam.
Johannes Lugenge (kushoto) na Promota wa pambano hilo kati ya Mada Maugo na Francsis Cheka, Lucas Rutahindurwa wakionesha mkanda wa Ubingwa wa I.B.F Afrika na gari atakalopewa bingwa wa mchezo huo siku ya pambano hilo. Picha na Super D.
*************************************
Na Mwandishi Wetu
WAANDAAJI wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka na Mada Maugo leo wameonesha rasmi gari na makanda watakalogombania Mabondia hao Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa la uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.
WAANDAAJI wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka na Mada Maugo leo wameonesha rasmi gari na makanda watakalogombania Mabondia hao Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa la uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Msemaji wa pambano hilo, Yasini Abdallah, alisema kuwa kuwekwa wazi kwa mkanda huo na Gari kuwa kunaashiria maandallizi yamekamilika na kupamba moto kwa pambano hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo.
“Tumeonysha gari na mkanda atakavyokaabidhiwa mshindi ili kuwathibitishia wadau wa ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa tupo makini na pambano hili na sio la kibabaishaji na kama tulivyosema awali kuwa majaji watoka nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe kulingana na hadhi ya mkanda,” alisema Kaike.
Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa siku hiyo hiyo ya pambano baada ya kutangazwa mshindi na kupewa mkanda.
Awali mabondia hao walishakutana na katika mapambano mawili tofauti ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi, ambapo Maugo hakukubali matokeo hayo na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.
Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha mawazo na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kibao DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo, Rajabu Mhamila ‘Super D’.
alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo. alisema Super D.
No comments:
Post a Comment