*YAZINDUA “HEINEKEN CHAMPIONS PLANET”
KWA AJILI YA WATEJA WAKE KUANGALIA MICHUANO YA LIGI YA UEFA*“Heineken Champions Planet” inalenga kuwapa
wateja wake na mashabiki wa Ligi ya Mabingwa ya
UEFA burudani ya kipekee.
*Heineken imekuwa ikishirikiana na UEFA tangu msimu wa 2004/05 imeahidi kuendelea kuwa mfadhili mkuu wa mashindano hayo hadi mwaka wa 2014/15.
Uzinduzi wa “Heineken Champions Planet” unatokana na mafanikio makubwa ya matembezi ya kombe la Ligi ya UEFA uliodhaminiwa na Heineken hapa nchini Tanzania na Kenya kutoka Machi 23 hadi Machi 31.
Ligi ya mabingwa ilianzishwa na UEFA mwaka wa 1992,
na imeelezzwa na wengi kuwa ni moja ya mashindano bora katika ulimwengu wa soka.
“Heineken Champions Planet” inliyozinduliwa jana ni jumba kubwa la kifahari lililopo mtaa wa Oysterbay.
Aidha “Heineken Champions
Planet” ina vyumba vingine vya michezo mbalimbali ambavyo vimewekewa PS3, meza za foosball, pool tables na chumba
kulicho andaliwa binafsi kwa wanahabari.
Meneja mkuu wa masoko Afrika mashariki, Krijin Jansen alisema “ Kama mshiriki wa muda mrefu wa Ligi ya Mabingwa la UEFA, Heineken inaelewa kuwa msisimko uliopo katika mashindano haya unahitaji mambo mbali mbali ya kuwachangamsha wateja wao, Kwa ushirikiano mkubwa waliotuonyesha “Heineken Champions Planet” imetekeleza miundo mbinu hii ya kipekee ili kuwaigiza mashabiki wake kwa njia thamani.
Kutokana na umaarufu wa Heineken kote duniani, bidhaa hii imezindua njia ya kuwashirikisha
wateja katika sehemu chaguliwa za usiku nafasi ya kufuraiya mashindano ya Ligi
ya Mabingwa la UEFA msimu wa 2011/12 hadi mwishoni 19 Mei katika “Heineken Champions Planet”.
No comments:
Post a Comment