Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na
Balozi wa Korea nchini, Young-Hoon Kim, wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi
rasmi wa Chuo kipya cha Ufundi Stadi cha VETA kilichojengwa Mkoa wa Lindi.
Uzinduzi huo ulifanyika jana. Kulia ni Mkurugenzi wa VETA,
Zebadia Moshi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akibonyeza 'Alam', kuashiria uzinduzi rasmi wa Chuo kipya cha Ufundi Stadi cha
VETA kilichojengwa Mkoa wa Lindi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Ghariub Bilal,
akisikiliza maelezo kuhusu jinsi ya ufundishaji wanafunzi kwa kutumia mtambo wa
kufua Umeme, kutoka kwa Mwalimu wa Umeme Veta, Majolo Mwigole, wakati Makamu
alipofika kuzindua Chuo hicho cha VETA mkoa wa Lindi jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Shukuru Kawambwa,
Balozi wa Korea nchini, Young-Hoon Kim na Viongozi wa VETA, wakati akitembelea
na kukagua baadhi ya majengo mapya yaliyojengwa ya Chuo cha Ufundi Stadi cha
VETA, baada ya kuzindua rasmi chuo hicho mkoa wa Lindi jana.
Makamu wa Rais, Dkt Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na Viongozi wa Serikali na viongozi wa Chuo hicho.
No comments:
Post a Comment