• Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Mazingira
  • Jamii
  • Siasa
  • Bunge
  • Habari Picha
  • Michezo
  • Burudani
SUFIANIMAFOTO

Habari za Punde

Home *MAXIMO AKUTANA NA RAIS KIKWETE NA KUMSHAURI JINSI YA KUPATA WACHEZAJI BORA WA TIMU YATAIFA

*MAXIMO AKUTANA NA RAIS KIKWETE NA KUMSHAURI JINSI YA KUPATA WACHEZAJI BORA WA TIMU YATAIFA

sufianimafoto Tuesday, April 17, 2012
 Kocha wa zamani wa Taifa Stars Marcio Maximo, ambaye kwa sasa anafundisha timu ya Democrata ya nchini Brazil,  akisalimiana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete, alipokwenda kumsalimia Rais katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo jana.
Kocha wa zamani wa Taifa Stars Marcio Maximo akimsalimu mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete alipokwenda kuwasalimia katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo.
*********************************************

Na Anna Nkinda – Sao Paul, Brazil
VILABU vya soka vya nchini Tanzania, vimeshauriwa kuwa na timu nzuri kuanzia ngazi ya watoto wenye umri wa miaka nane, vijana na kuendelea ili kupata timu bora ya Taifa.
Wito huo umetolewa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Star Marcio Maximo wakati akiongea na waandishi wa habari mjini Sao Paul.
Maximo alisema kuwa timu nyingi ambazo ni bora na zinafanya vizuri katika mchezo wa soka zimekuwa zikiwaandaa watoto wenye vipaji vya mchezo huo wangali wadogo ili waweze kuwa wachezaji wazuri hapo baadaye.
Kocha Maximo pia alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Jakaya Mrisho kikwete, ambapo alimnshukuru sana Rais kwa ushirikiano wa hali ya juu aliompa wakati alipokuwa akiifundisha Taifa Stars miaka takriban mitatu iliyopita.
Kwa upande wake Rais Kikwete alimpongeza Kocha Maximo kwa juhudi zake za kuendeleza soka la Tanzania, akimwambia uwepo kwake Tanzania kuliasidia sana kuiweka nchi katika ramani ya mchezo huo.
Rais Kikwete alikubaliana na kocha huyo kwamba ili timu ya Taifa ifanye vyema ni lazima maandalizi yaanzie ngazi za chini, ikiwemo vilabu kuwa na timu za watoto na vijana ambao baadaye watakuwa hazina ya Taifa Stars.
Kuhusiana na uvumi ulioenea kuwa anatakakwenda kufundisha timu za Taifa Stars, Azam na Yanga alisema kuwa siyo kweli na wala hajawasiliana na timu hizo na hawezi kwenda kufundisha kwani hivi sasa anamkataba wa kufundisha timu ya Democrata iliyopo nchini humo.
Rais alimshukuru Kocha Maximo kwa kuja kumsalimia na kumpa zawadi ya jezi ya timu ya Democrata anayofundisha, na kumtakia heri na fanaka katika kazi yake hiyo.
“Timu ya Taifa Star ina kocha mzuri ambaye ninamuheshimu na ninaukubali ufundishaji wake hivyo basi kupitia kocha huyo ninaamini watanzania watazidi kuendelea katika soka na kufika mbali zaidi”, alisema.
Maximo alimalizia kwa kusema kuwaanamawasiliano mazuri na watanzania na anawapenda ndiyo maana kila mahali anapopita anajivuna na kusema kuwa Tanzania ni nchi yake ya pili.
Hivi sasa Maximo ni kocha wa timu yaDemocrata iliyopo nchini humo ambapo wiki ijayo inatarajia kuanza mashindano ya taifa yatakayopelekea kupata wachezaji bora watakaoshiriki mashindano ya kombe la Dunia yanayotarajia kufanyika mwaka 2014 nchini Brazil.
 Rais Jakaya Kikwete, akipokea zawadi ya Jezi ya timu ya Kocha wa zamani wa Taifa Stars Marcio Maximo, ambaye kwa sasa anafundisha timu ya Democrata ya nchini Brazil,  alipokwenda kumsalimia Rais katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo jana.



  • Blog Comments
  • Facebook Comments

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

MATANGAZO MADOGO MADOGO

MAFOTO PRODUCTION & ENTERTAINMENT KWA MAHITAJI YAKO YA STILL PICTURE, VIDEO SHOOTING, MUSIC & Mc's KATIKA SHEREHE YA AINA YEYOTE. VIDEO EDDITING, COVER DISGNING, PPS ZA DK 3, POSTERS ZA AINA MBALIMBALI COVER CD PRINTING, BURNING CD N.K. WASILIANA NASI KWA NO, 0787 200005/0754, 0655-306109/0714 656660 BARUA PEPE:- muhidinuk@yahoo.co.uk,sufianimafotoblog@gmail.com AMA TEMBELEA www.sufianimafoto.com

BLOGU RAFIKI

  • JIACHIE
    WAPIGA KURA 37,647,235 KUPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29, 2025 - *Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na wananchi wakati akisoma risala yake kuhusu Uchaguz...
    42 minutes ago
  • MICHUZI
    Askofu Mwankenja ahimimiza watanzania kupiga kura Oktoba 29 - Na Mwandishi Wetu Askofu wa Kanisa la Furahini katika Bwana la jijini Dar es Salaam Dkt.Ezekiel Mwankenja amesema kuwa Watanzania kujitokeza katika kupiga ...
    9 hours ago
  • LENZI YA MICHEZO
    VIJANA KAHAMA WAJITENGA NA MAANDAMANO, WAAPA KULINDA AMANI UCHAGUZI MKUU - Na Neema Nkumbi, Kahama Vijana wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamekataa kushiriki maandamano yaliyopangwa kufanyika siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 29, ...
    12 hours ago
  • MTAA KWA MTAA BLOG
    UDAHILI WA WANAFUNZI WA TIBA KUONGEZEKA MARA TATU CHUO CHA MUHAS KUPITIA MRADI WA HEET - Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ( MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa, akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 27,2025 D...
    13 hours ago
  • Wazalendo 25 Blog
    Elimu : Bajeti za Elimu Zisipuuzwe wakati wa misukosuko ya Kiuchumi na Kisiasa Duniani - Kikwete na Malala Waonya. - Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Malala Yousafzai, wameonya juu ya mwenendo hatarishi duniani wa kupunguza au ku...
    1 week ago
  • LUKAZA
    UNESCO Yaunga Mkono Juhudi za Serikali Kuboresha Mfumo wa Usimamizi wa Mafunzo Endelevu ya Walimu (MEWAKA) - [image: Picture1] [image: Picture2] [image: Picture3] [image: Picture4] [image: Picture5] Na Mwandishi Wetu, Arusha. Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekno...
    1 month ago
  • PAMOJA
    Ecobank yasherehekea miaka 40 kwa kampeni ya “Gutuka na Ecobank” - Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Wateja Binafsi Ecobank Tanzania, Innocent Urio (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampeni maalum ...
    1 month ago
  • BIN ZUBEIRY
    TAIFA STARS YACHAPWA 1-0 NA NIGER ZANZIBAR KUFUZU KOMBE LA DUNIA - TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jana ilichapwa bao 1-0 na Niger pungufu katika mchezo wa Kundi E kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2026 Uwanj...
    1 month ago
  • TZA
    Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025 - Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania March 3, 2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma Magazetini ke...
    7 months ago
  • BongoCelebrity
    - [image: Tumore prostatico: la prognosi in base a stadio, grado e rischio] Tumore prostatico: la prognosi in base a stadio, grado e rischio alt=”” class=”w...
    1 year ago
  • HABARI NA MATUKIO
    BODI YA MAJI BONDE LA KATI YAWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI KUFUATIA MAFURIKO KWENYE MAZIWA YA KINDAI, MUNANG NA SINGIDANI - * Mhandisi Rasilimali za Maji, Bodi ya Maji Bonde la Kati, Moses Salumbi (kushoto), akiweka alama za ukomo wa maji ya mafuriko kwenye Maziwa ya Kindai na...
    5 years ago
  • Mzuka wa Fungo
    MSANII DIAMOND AZINDUA WIMBO WA COLOURS KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI - Cathbert Kajuna To:amichuzi,othmanmichuzi,MUHIDIN MICHUZI,Geofrey Adroph Bcc:fungoomar@yahoo.com May 15 at 6:00 AM Msanii Diamond akipagawisha mashabiki wa...
    7 years ago
  • MTOTO WA KITAA
    RAIS JOHN MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA JCA NA BALOZI WA JAPAN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM - *Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Shini...
    8 years ago
  • NASMAMAFOTO
    JOSE MOURINHO HAS REPORTEDLY 'SHOKED' SOME OF HIS MANCHESTER UNITED PLAYERS - *Jose Mourinho might have hoped for a longer honeymoon at Manchester United, but three defeats in a row, in the space of a week, have led to the first maj...
    9 years ago
  • Mbeya Yetu
    TIBA YA MAGONJWA YAKO NA MATATIZO MBALIMBALI SASA HII HAPA BEI NAFUU SOMA HAPA KWA MAKINI - Je? Unaumwa au unasumbuliwa na matatizo yoyote kiafya? Unahitaji msaada wa haraka, tuna virutubisho sahihi kuondoa magonjwa kama kisukari, presha, uvimb...
    9 years ago
  • Bongo Newz Corner
    DIAMOND PLATINUMZ HOUSE 'STATE HOUSE' - Bila shaka muziki unalipa na ndio maana mwanamuziki wa Bongo Fleva, kutoka Tanzania Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz, ameweza kujenga nyumba jambo ambal...
    10 years ago
  • NEW HABARI BLOGSPOT.COM
    SIMBA ILIPOWASHANGAZA MASHABIKI WA SOKA JANA,ILIPOCHOMOA MABAO 3 NA KULAZIMISHA SARE YA 3-3 - * Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro', akiwania mpira na kipa wa Simba Abel Dhaira, wakati wa kipindi cha pili cha mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanza...
    12 years ago
  • Maisha Yetu
    -
  • MTANZANIA HALISI
    -
  • K-VIS BLOG
    -
  • Saluti5- Tanzania
    -

WALIOTEMBELEA BLOG HII

Followers

Labels

  • BUNGE
  • Burudani
  • HABARI PICHA
  • Habari
  • Michezo
  • Siasa

Zilizosomwa Zaidi

  • TUWAPE FARAJA FAMILIA ZENYE WATOTO WENYE USONJI, TUSIWATENGE -JACKLINE MJEMA
      Mwandishi na Mtunzi wa Vitabu, Jackline Christopher akionesha kitabu chake cha All the Colors I See baada ya kukizindua mapema wiki hii am...
  • TAMASHA LA KARIAKOO FESTIVAL LAZINDULIWA DAR NMB WAISHIKA KARIAKOO
    Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Toba Nguvila (kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, A...

SUFIANIMAFOTO Mafoto Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.