Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kesho inaingia raundi ya 23, ambapo itachezwa jumla ya mechi nne.
Polisi Dodoma wataikaribisha Azam kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini
Dodoma wakati JKT Ruvu watakuwa wageni wa Mtibwa Sugar mjini Turiani.
Mechi nyingine
za raundi hiyo zitakuwa kati ya Kagera Sugar na African Lyon zitakazooneshana
kazi kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Nayo Moro United inaikaribisha
Oljoro JKT katika mechi itakayofanyika Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Raundi ya 23
itakamilika Jumapili (Aprili 15 mwaka huu) kwa mechi kati ya Ruvu Shooting na
Simba itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Yanga itakuwa mgeni
wa Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Villa Squad
itapambana na Coastal Union kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Ligi hiyo
itaendelea tena Aprili 18 mwaka huu kwa mechi tano. Kagera Sugar vs Yanga mjini
Bukoba, Toto Africans vs African Lyon jijini Mwanza, JKT Ruvu vs Simba- Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam, Ruvu Shooting vs Moro United mjini Mlandizi na Polisi
Dodoma vs Coastal Union mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment