Mechi ya Ligi ya Vodacom kati ya Simba na Moro United iliyokuwa ichezwe
Aprili 5 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam isogezwa mbele hadi
Jumatatu ya Aprili 23 mwaka huu kwenye uwanja huo huo na itaanza saa 1 kamili
usiku.
Mabadiliko hayo yamefanyika ili kuipa Simba fursa ya kujiandaa vizuri
kwa mechi yao ya Kombe la Shirikisho la Afrika dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan
itakayochezwa Aprili 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10
kamili jioni.
Pia mechi kati ya Azam na Mtibwa Sugar iliyokuwa ichezwe Aprili 21 mwaka
huu kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam imesogezwa mbele hadi Aprili 22
mwaka huu kupisha mechi ya U20 kati ya Tanzania na Sudan itakayochezwa Aprili
21 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi nyingine mbili zimefanyiwa marekebisho, Coastal Union na Kagera
Sugar zilizokuwa zicheze jijini Tanga, Aprili 29 mwaka huu, mechi yao
imesogezwa hadi Aprili 30 mwaka huu ili kupisha shughuli za Mei Mosi kwenye
Uwanja wa Mkwakwani.
Nazo Azam na Toto Africans zilizokuwa zicheze Aprili 26
mwaka huu Uwanja wa Chamazi, sasa zitacheza Aprili 28 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment