Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kesho
(Aprili 18 mwaka huu) itafungua maombi ya tenda zilizowasilishwa na kampuni
mbalimbali kwa ajili ya kutengeneza tiketi za elektroniki.
Maombi hayo yatafunguliwa saa 9 alasiri kwenye ofisi za TFF ambapo
kampuni zote zilizowasilisha tenda zinatakiwa kuwepo wakati wa ufunguzi huo.
Machi 9 mwaka huu TFF ilitangaza tenda kwa ajili ya kutengeneza tiketi za
elektroniki kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom na mechi nyingine
inazozisimamia.
No comments:
Post a Comment