Habari za Punde

*UFUNGUZI WA KONGAMANO LA MAKATIBU MUHTASI WAFANYIKA JIJINI MWANZA LEO


Mgeni Rasmi katika Kongamano la Makatibu Muhtasi nchini lililofanza leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Malaika Jijini Mwanza,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu (katikati) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Eng.Evarist Ndikilo pamoja na wadau wengine wa Kongamano hilo wakati akiwasili kufungua kongamano hilo leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Pili Penda, akitoa maelezo kuhusu Kongamano hilo kwa Mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu wakati wa ufunguzi uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika Beach Resort, Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa Mwanza,Eng.Evarist Ndikilo akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo la Pili la Makatibu Muhtasi nchini Tanzania (2th National Secretarial Confrerence).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la Makatibu Muhtasi nchini Tanzania (2th National Secretarial Confrerence) linaloendelea hivi sasa kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika Beach Resort,Jijini Mwanza.
Muwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Mama Wanderage akitoa salamu za Mkuu huyo wa Chuo kwa Makatibu Muhtasi waliopo kwenye Kongamano hilo.
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Pili Penda akimkabidhi zawadi ya Tuzo ya heshima Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu kwa uwepo wake kwenye Kongamano hilo leo. 
Dk. Mary Nagu akisalimiana na Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo.
Ephraim Kibonde MC mwendesha shughuli hiyo ya Kongamano akiwa kazini. 
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo.
Washiriki wa Kongamano hilo wakifurajia jambo.
Ukumbi huo ulifurika kama hivi.
Picha ya pamoja ya kumbukumbi baada ya kufunguliwa kwa kongamanao hilo.



--
 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.