Mshambuliaji wa Timu ya Taifa na timu ya TP Mazembe, Thomas Ulimwengu (kushoto) akikokota mpira wakati akiwa katika moja ya mchezo wa timu ya Taifa hivi karibuni.
*********************************
MSHAMBULIAJI
Thomas Ulimwengu ambaye ndiye mchezaji pekee kutoka nje aliyeitwa na Kocha Kim
Poulsen kwenye U20 (Ngorongoro Heroes) anatarajia kujiunga na kikosi hicho
ambacho kiko kambini kesho.
Ulimwengu ambaye
anachezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) atawasili
kesho saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways akitokea jijini Lubumbashi.
Ngorongoro
Heroes ambayo iliingia kambini Aprili 20 mwaka huu inajiandaa kwa mechi ya
mashindano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 dhidi ya Sudan.
Mechi hiyo itachezwa Aprili 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kuanzia saa 10 kamili jioni.
Kwa mujibu wa
Kocha Poulsen, kikosi chake kesho (Aprili 14 mwaka huu) kitakuwa na awamu
(sessions) mbili za mazoezi kwenye Uwanja wa Karume. Awali ya kwanza itakuwa
asubuhi na ya pili itafanyika jioni.
Wachezaji
wengine walioko kwenye kikosi hicho cha Ngorongoro Heroes ni Saleh Malande,
Aishi Manula, Hassan Kessy, Said Ruhava, Carlos Kilenge, Dizzana Issa, Amani
Kyata, Issa Rashid, Emily Mgeta na Khamis Mroki.
Wengine ni
Ramadhan Singano, Frank Sekule, Frank Domayo, Omega Seme, Abdallah Hussein,
Ibrahim Rajab, Hassan Dilunga, Alhaje Zege, Jerome Lambele, Atupele Green na
Simon Msuvan.
Mechi ya
marudiano dhidi ya Sudan itachezwa jijini Khartoum kati ya Mei 4, 5 na 6 mwaka
huu.
Fainali
za Afrika kwa vijana zitafanyika Machi mwakani nchini Algeria. Timu nne za juu
kwenye fainali hizo zitacheza Fainali za Dunia zitakazofanyika nchini Uturuki
kuanzia Juni hadi Julai
No comments:
Post a Comment